Kuhusu mafunzo
Mafunzo haya ya mtandaoni iitwayo “Utangulizi wa kushughulikia watoto waliopitia ukatili wa kingono katika hali ya mgogoro wa kibinadamu (kipindi cha 2)” (maarifa ya awali ya PES) inalenga kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya kuimarisha uwezo katika eneo hili. Yameandaliwa ili kuwapa washiriki maarifa ya msingi juu ya PES kwa kutegemea sura ya 1 na 2 ya toleo jipya la rasilimali zinazohusu PES (Mwongozo na Mafunzo, toleo la 2, 2023). Pia yanaweza kutumika kama mafunzo ya kupiga msasa na kuwa sharti kwa watu wanaotaka kushiriki mafunzo ya ana kwa ana kuhusu PES.
Malengo ya kujifunza
Baada ya mafunzo, washiriki:
- Wataweza kuelewa katika muktadha wao ukatili wa kingono dhidi ya watoto;
- Wataelewa mbinu ya PES katika usimamizi wa kesi;
- Watafahamu kanuni kuu za PES;
- Wataweza kutambua na kuwasilisha nyanja kuu za maarifa yanayohusiana na ukatili wa kingono dhidi ya watoto.

Walengwa
- Wafanyakazi wanaohusika katika usimamizi wa kesi za ulinzi wa watoto na ukatili wa kijinsia katika hali za kibinadamu;
- Watoa huduma wengine wanaotoa msaada na huduma kwa watoto waliopona ukatili wa kingono (hasa huduma za afya au huduma za kisheria), na wanaoweza pia kufaidika na rasilimali zinazohusiana na PES.
Muda
~masaa 4
Mbinu
Kujifunza kwa kujitegemea
Muundo
- Mbinu ya PES – Misingi na kanuni kuu
- Nyanja kuu za maarifa
Mtu wa kuwasiliana
Kwa maswali yanayohusiana na maudhui tafadhali wasiliana nasi Alexia Nisen, Kitengo cha ulinzi wa watoto, anisen@unicef.org
Kwa maswali yote kuhusu mafunzo au kipengele chochote cha kiufundi, tafadhali tuma barua pepe kwa agora@unicef.org